Highlights

Wakazi wa kaunti ya Marsabit watoa hisia mseto kuhusu ombi la serikali kutaka msaada wa kutatua janga la njaa.

Wakaazi wa Kaunti ya Marsabit wametoa maoni yao kuhusu hatua ya serikali kuomba msaada kutoka kwa wahisani ili kukabiliana na makali ya ukame na njaa.

Baadhi ya wakaazi waliozungumza na kituo hiki wamesema ni jambo la kushangaza kuona serikali ikiomba msaada ilhali imekuwa ikitumia pesa nyingi katika miradi mingine bila kuonyesha kuwa kuna uhaba wa fedha. Wamesisitiza kuwa jukumu la serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata chakula, hasa wakati wa majanga kama ukame.

Kwa upande wake, mtaalamu wa masuala ya kifedha Eric Mugambi amesema ni wajibu wa serikali kuhakikisha raia wake wanakuwa na usalama wa chakula. Ameeleza kuwa kwa muda mrefu suala la maandalizi dhidi ya ukame limekuwa likipuuzwa. Kulingana naye, uhaba wa chakula kwa wananchi na lishe kwa mifugo ni janga linaloweza kutokea, na serikali inapaswa kuwa na mikakati madhubuti ya kukabiliana nalo mapema.

Serikali inasema inahitaji shilingi bilioni saba kusaidia chakula, maji na dawa kwa waathiriwa kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo, huku bilioni sita zikihitajika kusaidia mifugo. Kaunti kumi zinazoathirika zaidi na zinazohitaji msaada wa haraka ni Mandera, Wajir, Garissa, Kilifi, Kitui, Marsabit, Kwale, Kajiado, Isiolo na Tana River.

Kaunti nyingine zilizoathirika na ukame ni Samburu, Turkana, Taita Taveta, West Pokot, Tharaka Nithi, Embu, Nyeri, Laikipia, Narok, Baringo, Makueni, Meru pamoja na Lamu.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment