Polisi wawili na raia mmoja washtakiwa kwa wizi wa ushahidi Marsabit.
Maafisa wawili walio na hadhi ya konstabo pamoja na raia mmoja wameshtakiwa katika mahakama ya Marsabit kwa kosa linalofunagamana na wizi wa mali iliyofaa kutumika kama ushahidi.
Mahakama imearifiwa kuwa kati ya tarehe 13 na 18 mwezi Aprili mwaka 2025 katika kituo cha Marsabit, washukiwa hao konstabo David Kiragu, konstabo Amos Bett na raia Andrew Wanyonyi walivunja chumba cha kuhifadhi ushahidi na kuiba katoni 25 za pombe zenye thamani ya shilingi 72,500.
Pombe hiyo ilikuwa ushahidi katika kesi mmoja katika mahakama ya Marsabit.
Hapo jana Jumatatu mbele ya hakimu mwandamizi wa mahakama ya Marsabit Simon Arome washukiwa hao ikiwemo Wanyonyi ambaye amekuwa kizuizini kwa miezi nane, walikana mashitka dhidi yao na kuachiliwa kwa dhamani ya pesa taslimu shilingi 10,000.
Kesi hiyo itaamuliwa 29 mwezi huu wa Disemba.



Post Comment