Highlights

Jamaa afikishwa mahakamani Marsabit kwa tuhuma za kutishia kumwangamiza mwenzake.

NA NYABANDE ORWA

Jamaa mmoja amefikishwa katika Mahakama ya Marsabit kwa tuhuma za kumtishia mwenzake kumwangamiza yeye na watoto wake.

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Marsabit, Simon Arome, mshukiwa Hussein Sode anatuhumiwa kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya mlalamishi Dade Adan katika lokesheni ya Nagayo tarehe saba mwezi huu wa Desemba, akidaiwa kusema kuwa angemdunga kisu yeye pamoja na familia yake.

Katika shtaka la pili, mshukiwa Sode anatuhumiwa kutumia maneno ya matusi dhidi ya mlalamishi kama njia ya kumdhalilisha.

Hata hivyo, mshukiwa amekana tuhuma zote dhidi yake.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena tarehe 13 mwezi ujao wa Januari mwakani.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment