Highlights

Wakaazi wa kubi qoti maikona walia ukosefu wa maji, waomba viongozi kuwasaidia.

NA Samuel Kosgei

Wakaazi wa Manyatta ya Kubi Qoti iliyo wadi ya Maikona eneobunge la North Horr kaunti ya Marsabit wametoa ombi kwa viongozi wa serikali kuu, serikali ya kaunti au hata mashirika ya kibinafsi kuwapa msaada wa maji kwani makali ya kiu yanawaumiza sana.

Wakaazi hao wakiongozwa na Stephen Ali Gorai wanasema kuwa kutokana na kiangazi cha muda mrefu na mvua za vuli kukosa kunyesha mwaka jana, hali imekuwa mbaya kutokana visima tegemeo kukauka.

Sehemu ambapo maji inapatikana ni zaidi ya kilomita 30 hivyo kuzidisha mahangaiko ya wananchi.

Sasa wanatoa wito kwa asasi husika za serikali kuwapalekea maji.

Gorai aidha anasema kuwa imekuwa vigumu kuwapata viongozi wao kutokana na madai ya kutopokea simu na pia ukosefu wa mtandao wa simu.

Anasema kwa sasa inawabidi kujikusanya kama majirani na kutafuta mbinu isiyokuwa rahisi kusaka maji kiasi ya matumizi.

Vijiji vya karibu kama vile Bori, Forole , Shankera, Waara, Hurri hills, Baqaqa pia anasema inapitia matatizo sawa na wao.

Post Comment