Highlights

Ipoa yaanzisha uchunguzi wa kisa cha kushambuliwa kwa mtoto loiyangalani.

NA JB Nateleng/Nyabande Orwa

Familia ya kijana wa miaka 13 anayedaiwa kujeruhiwa kwa risasi wakati wa oparesheni ya kiusalama katika eneo la Sarima, wadi ya Loiyangalani, mapema mwezi huu, imeitaka idara ya usalama katika kaunti ya Marsabit kuharakisha uchunguzi na kumchukulia hatua afisa anayehusishwa na tukio hilo.

Wakizungumza na idhaa hii, familia hiyo imetoa wito kwa mamlaka ya kusimamia utendakazi wa polisi (IPOA) kuanzisha uchunguzi wa kina ili kuhakikisha haki inatendeka kwa kijana huyo na familia yake.

Aidha, wameitaka serikali kusaidia kurejesha mifugo inayodaiwa kuibwa wakati wa oparesheni hiyo.

Akizungumza na kituo hiki, kamanda wa polisi wa kaunti ya Marsabit, Leonard Kimaiyo, amesema kuwa kesi hiyo kwa sasa iko chini ya uchunguzi wa IPOA.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment