Highlights

Wakaazi Marsabit Central watoa hisia mseto kuhusu pendekezo la kufuta ushuru wa mishahara kwa wakenya wa kipato cha chini ya shilingi 30,000

NA JB Nateleng

Baadhi ya wakaazi wa Marsabit Central, eneo bunge la Saku, wamepongeza mpango wa serikali ya Rais William Ruto wa kufutilia mbali ushuru wa mishahara kwa wakenya wa kipato cha chini ya shilingi 30,000

Wakizungumza na Shajara wakaazi hao wametaja pendekezo hilo kuwa la afueni kwa wafanyikazi milioni 1.5 haswa wakati huu ambapo gharama ya maisha iko juu.

Vielvile wameitaka serikali ya kenya Kwanza kuboresha uchumi na kubuni nafasi za ajira kwa vijana.

Aidha kuna wale wanaohisi kuwa pendekezo hilo ni mpango wa kisiasa tu haswa kuelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Serikali pia inapanga kupunguza ushuru kwa wafanyikazi wanaopata mshahara wa hadi shilingi 50,000 kutoka ushuru wa  asilimia 30% hadi asilimia 25%.

Akizungumza hapo jana katika Ikulu ya Rais alipokuwa akiwakaribisha wagombea wa UDA, Ruto amesema hatua hiyo itasaidia kulinda wananchi kutokana na changamoto za kifedha zinazojirudia kwa kuongeza mapato yanayoweza kutumika.

Post Comment