Wafugaji waendelea kuhimizwa kuchukua tahadhari msimu huu wa mvua
Na JB Nateleng
Wito umetolewa kwa wafugaji kuchukua tahadhari wakati huu ambapo idara ya utabiri wa hali ya anga nchini (MET) imetabiri kuwa maeneo mengi jimboni yataendelea kupokea mvua.
Akizungumza na Shajara Chifu wa lokesheni ya Lontolio Lawrence Lpatirian amewahimiza wafugaji wanaoishi katika maeneo yaliyo chini ya milima ama karibu na mito kuhamia kwenye maeneo salama ili kuepuka hatari.
Chifu Lawrence ametoa wito kwa wazazi kuweza kuwachunga wanao dhidi ya kucheza karibu na mito akisema kwamba hili linahatarisha maisha yao.
Kauli yake imesisitizwa na naibu chifu wa Moyale Township Yusuf Jaldesa ambaye amesema kuwa wakulima wanakabiliana na changamoto ya kupata mbegu kwa ajili ya kilimo msimu huu wa mvua.



Post Comment