Highlights

Wazazi Laisamis watakiwa kupeleka watoto shuleni

Na Nyabande Orwa

Naibu Kamishna wa Kaunti ndogo ya Laisamis, Kepha Mwaribe, amewataka wazazi kuhakikisha watoto waliotimiza umri wa kwenda shule wanapelekwa shuleni.

Mwaribe amesema kuwahusisha watoto katika kuchunga mifugo mapema kunaharibu mustakabali wao na kunaweza kuwaingiza katika vitendo vya wizi wa mifugo pamoja na makundi haramu yanayochipuka kutokana na ukosefu wa elimu.

Wakati huo huo, amesema kuwa ukosefu wa elimu umechangia baadhi ya watu kukata miti ovyo bila kufahamu umuhimu wake katika kuhifadhi mazingira.

Amesisitiza kuwa ni jukumu la serikali kuhakikisha watoto wote wako shuleni, na kuwaonya wazazi watakaoshindwa kutimiza wajibu huo kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.

Naibu Kamishna huyo alikuwa akizungumza Jumanne katika maadhimisho ya siku ya wanyamapori duniani yaliyofanyika katika hifadhi ya Losai, Laisamis.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment