Highlights

Mtaala wa CBE waendelea kukumbatiwa Marsabit huku michezo ya shule za upili ikanza.

Na JB Nateleng

Msimamizi wa ubora wa elimu katika Kaunti ya Marsabit, Mumas Wanyama, amesema mtaala wa umilisi (CBE) unaendelea kukumbatiwa zaidi katika kaunti hii. Amewataka walimu na wadau wa elimu kushirikiana ili kuhakikisha utekelezaji wake unafanikiwa.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya muhula wa kwanza ya shule za upili katika kitengo cha kaunti yaliyofanyika katika Shule ya Moi Girls, Wanyama amesema wengi wa washiriki ni wanafunzi wa Gredi ya 10, jambo linaloonyesha kuwa mtaala huo unaendelea kukubalika.

Wakati uo huo, mwenyekiti wa muungano wa walimu wakuu wa shule za upili (KESSHA) katika Kaunti ya Marsabit, Halima Adan, amesema walimu wakuu wanaendelea kujitahidi kuhakikisha mtaala wa CBE unatekelezwa kikamilifu.

Naye mwenyekiti wa michezo ya shule za upili katika Kaunti ya Marsabit, Ibrahim Gere, amewataka wanafunzi kudumisha nidhamu na kufuata utaratibu sahihi wanapowasilisha malalamishi.

650822351_1400625175412565_1296318930780631092_n-1024x683 Mtaala wa CBE waendelea kukumbatiwa Marsabit huku michezo ya shule za upili ikanza.
Kutoka kushoto kuenda kulia: Mumas Wanyama William Kamuguna pamoja na Ibrahim Gere.

Kauli hiyo imeungwa mkono na mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Marsabit, William Kamuguna, ambaye amesema kuwa mashindano hayo ni ya wanafunzi, hivyo ni muhimu wapewe muda na nafasi ya kuonyesha na kukuza vipaji vyao.

Mashindano hayo ya muhula wa kwanza katika kitengo cha kaunti yalianza leo na yanatarajiwa kukamilika kesho, huku washindi wakitarajiwa kuwakilisha Marsabit katika mashindano ya mkoa yatakayofanyika wiki ijayo katika Kaunti ya Meru.

Post Comment