Highlights

Seneta Chute aitaka Seneti kuchunguza uchimbaji wa bwawa la Moyam

Na Sabalua Moses

Seneta wa Marsabit Mohamed Chute ametaka uchunguzi ufanywe kuhusiana na uchimbaji wa bwawa na shughuli zinazohusiana na maendeleo katika eneo la Moyam lililoko eneo la BadanRero eneo bunge la Moyale kaunti ya Marsabit.

Akizungumzia suala hilo mbele ya Seneti, seneta huyo alibainisha kuwa Moyam ni eneo la malisho la msimu wa kiangazi linalosaidia wafugaji wakati wa ukame.

Aliibua wasiwasi kwamba ripoti ya uchimbaji wa kisima na kazi zinazohusiana—zinazodaiwa kuhusishwa na serikali ya kaunti jirani—huenda zilivamia ardhi ya malisho ya jamii, na hivyo kutia hali ya wasiwasi katika eneo hilo.

Chute aliitaka Kamati ya Seneti kuhusu Ardhi, Mazingira na Maliasili kubaini ikiwa idhini sahihi zilipatikana na kuhakikisha shughuli zozote ambazo hazijaidhinishwa zinasitishwa.

Pia alizitaka mamlaka, ikiwamo Tume ya Kitaifa ya Ardhi, kuharakisha usajili wa ardhi ya jamii kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi ya Jamii community land act, 2016 ili kulinda maeneo ya malisho ya wafugaji.

Post Comment