Wakaazi Loglogo waiomba serikali kujenga daraja Mto Sabamba
Na Caroline Waforo
Wakaazi wanaoishi karibu na Mto Sabamba ulioko katika eneo la Loglogo, eneobunge la Laisamis kaunti ya Marsabit wameiomba serikali kujenga daraja katika eneo hilo ili kuwawezesha kuendelea na shughuli zao za kila siku hasa wakati wa msimu wa mvua.
Wakizungumza na wanahabari wakaazi hao wakiongozwa na Diboya Idris wamesema kuwa mto huo ni hatari kuvukwa wakati wa mvua kwani maji hujaa na kuwazuia baadhi yao kushindwa kufika mjini hata nyakati za dharura.
Aidha, baadhi yao wamesema kuwa hawawezi kuhama makao yao na kuelekea katika nyanda za juu hali inayohatarisha maisha yao iwapo mvua kubwa itashuhudiwa katika eneo hilo.



Post Comment