Highlights

Vita dhidi ya mihadarati ni jukumu la kila mmoja- asema mratibu wa nacada marsabit.

NA Joseph Muchai

Vita dhidi ya mihadarati, dawa za kulevya pamoja na pombe haramu ni jukumu la kila mmoja katika jamii ya Marsabit.

Kwa mujibu wa Mratibu wa Mamlaka ya kukabiliana na dawa za kulevya NACADA tawi la Marsabit, Mohamed Waqo, ni muhimu katika kujumuisha walimu, wanafunzi pamoja na wazazi katika vita hivyo.

Amesema kuwa mamlaka hiyo imekuwa ikihimiza walimu kuwasaidia wanafunzi wanaotumia mihadarati kurekebisha mienendo yao badala ya kuwafurusha shuleni.

Aidha amewataka wazazi kuwa makini kwa kutambua dalili za mapema za matumzii ya mihadarati miongoni mwa watoto wao.

Wakati huo huo Waqo amesema kuwa wamekuwa wakifanya ziara katika shule mbalimbali kuwahamasisha wanafunzi kuhusu madhara ya matumizi ya dawa za kulevya na pombe haramu.

Kwa mujibu wa mratibu huyu shughuli za uhamasishaji zitarejelewa katika juma la pili la mwezi ujao humu jimboni Marsabit.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment