KEPSHA, KNUT zaitaka serikali kusaidia wanafunzi wa gredi ya 10.
NA Nyabande Orwa
Katibu mkuu wa chama cha kitaifa cha walimu (KNUT) tawi la Kaunti ya Marsabit, Rosemary Talaso, ameitaka serikali kuongeza mgao wa fedha za capitation shuleni ili kuhakikisha kila mwanafunzi anapata mazingira bora ya kusomea.
Akizungumza na kituo hiki, Talaso amesema ni hatua nzuri kwa Rais William Ruto kuagiza wanafunzi wote warudi shuleni hata bila sare rasmi na bila karo, hasa wale kutoka familia maskini. Hata hivyo, amesisitiza kuwa serikali ina wajibu wa kuhakikisha wanafunzi hao wanapata mahitaji ya msingi kama vile chakula na vifaa vya masomo.
Wakati huo huo, baadhi ya wazazi waliozungumza na kituo hiki wameunga mkono agizo la kuwapeleka watoto shuleni, lakini wameitaka serikali kuhakikisha mtaala wa CBC unaeleweka vyema kwa wanafunzi, walimu na wadau wengine wa elimu.
Kwa upande wake, Muungano wa walimu wakuu wa Shule za upili (KEPSHA) tawi la Isiolo, umeitaka serikali kuangazia kwa dharura suala la wanafunzi wanaojiunga na Gredi ya 10. Muungano huo unataka fedha zitolewe kusaidia lishe ya wanafunzi hao watakaojiunga na shule za upili bila kuchangia karo.
Mwenyekiti wa KEPSHA Isiolo, John Boscho Akale, amesema elimu ni jukumu la pamoja na kwamba wazazi, serikali na wadau wengine lazima washirikiane kuhakikisha watoto wanapata elimu bora.



Post Comment