Highlights

Ukame Marsabit watishia kuchochea ongezeko la matumizi ya mihadarati

Huku kaunti ya Marsabit ikiendelea kukabiliana na athari za ukame, hofu imeibuka kuwa matumizi ya dawa za kulevya na pombe haramu huenda yakaongezeka.

Kulingana na Mratibu wa Mamlaka ya kukabiliana na dawa za kulevya NACADA tawi la Marsabit, Mohammed Wako, changamoto za maisha zinazotokana na ukame huwafanya baadhi ya watu kugeukia mihadarati na pombe haramu kama njia ya kujiliwaza.

Wako anasema kuongezeka kwa matumizi ya mihadarati kunaweza kusababisha matatizo mengine ya kijamii ikiwemo matatizo ya afya ya akili.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment