Highlights

Jamii za wafugaji Loiyangalani zatakiwa kuvumiliana wanapokuwa katika sehemu za malisho.

NA JB Nateleng

Chifu wa Lokesheni ya Mt Kulal, eneo wadi ya Loiyangalani, Kaunti ya Marsabit Hosea Lemoni ametoa wito kwa wafugaji wote katika eneo la Loiyangalani kushirikiana na kuheshimiana wakati wanapochunga mifugo yao kwenye sehemu za malisho.

Amesema, iwapo kuna jamii zinahisi kwamba sehemu zao za malisho ni chache na wanapenda kuvuka mipaka ya jamii nyingine, ni muhimu wahakikishe wanafuata utaratibu unaofaa.

Hii itajumuisha kutuma wazee wa jamii zao kuzungumza na jamii zinazopakana ili kufikia makubaliano juu ya matumizi ya nyasi na vyanzo vya maji yenye kutosha.

Chifu Lemoni amesema kwamba kufikia sasa jamii ya wafugaji katika eneo hilo imeweza kukumbatia masomo ya watoto kwa kuwapeleka watoto wote shuleni.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment