Highlights

Idadi kubwa ya vijana gerezani marsabit yahusishwa na matumizi wa dawa za kulevya.

Na Caroline Waforo

Utumizi wa dawa za kulevya miongoni mwa vijana unaendelea kuwa donda sugu katika kaunti ya Marsabit, hali inayochangia kuongezeka kwa kesi zinazohusisha vijana hao mahakamani, nyingi zikiwa ni za kusababisha vurugu au kuvunja amani.

Kwa mujibu wa Hakimu Mkaazi wa Mahakama ya Marsabit Christine Wekesa, idadi kubwa ya vijana wanaokamatwa na kufikishwa mahakamani hujipata mikono mwa sheria kutokana na kujiingiza katika utumizi wa dawa hizo.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake siku ya hapo jana Jumanne, Hakimu Wekesa amesema kuwa vijana hawa ndio wanajumuisha idadi kubwa ya wafungwa walioko katika gereza la Marsabit.

Vilevile, Hakimu Wekesa ameitahadharisha jamii dhidi ya kutatua kesi zinazohusu dhulma za watoto pamoja na zile za jinai kule mashinani.

Kesi hizi pia haziwezi kutatuliwa kupitia njia mbadala ya sheria maarufu AJS

Hata hivyo Hakimu Wekesa amedokeza kuwa utekelezwaji wa mfumo mbadala wa AJS katika kesi zinazoruhusiwa kisheria, umechangia pakubwa katika kupunguza mrundiko wa kesi katika mahakama ya Marsabit.

Post Comment