Local Bulletins

Viongozi wa Turkana wataka raia kupewa silaha ili kujilinda kwa kuhisi serikali imeshindwa

Na Ken Simiyu

Kwa kauli moja sasa viongozi wa kaunti ya Turkana sasa wanaitaka serikali kurejesha silaha kwa maafisa wa akiba ili kupiga jeki juhudi za kukabiliana na utovu wa usalama. Wakirejelea mauaji ya hivi punde Zaidi viongozi hao wanasea kuwa visa vya kuchomwa kwa magari na wahalifu hii sio kitu kipya huku serikali ikiendelea kutazama tu.

Mbunge wa Turkanà mashariki Nicholas Ngikor ameshutumu vikali mauaji ya maafisa wa usalama na wahalifu katika kaunti ya Turkana. Ngikor anataika serikali kutopoteza muda wa kutuma maafisa wa usalama kuuana bure.

Hii leo asubuhi mtu mmoja ameuawa katika makabiliano mengine kati ya wahuni na raia katika eneo la Lokwamosing, Turkana Mashariki.

Adhuhuri ya leo wahuni hao wamekuwa wakikabiliana mirindimo ya risasi ikisikika siku nzima.

Hali ya wasi wasi ingali inashihudiwa maeneo ya Turkana kusini huku usafiri ukiathirika.

Mwili wa afisa alioripotiwa kupotea umepatikana msituni ukiwa na majiraha mabaya ya risasi.

Naye mwanaume mwengine aliye jitambulisha kutoka Nakwamekwi akipatikana baada ya siku tatu akiwa na jiraha la risasi, amesema kwamba alipigwa akiwa kwenye pikipiki huku pikipiki ikichukuliwa na wahuni hao.

 

 

 

Subscribe to eNewsletter