Local Bulletins

Shule zasalia kufungwa Turkana huku mwalimu mmoja mjamzito akibakwa na majangili wanne

Na Ken Simiyu

Kufuatia hali mbaya ya usalama katika eneo ya loyapata kainuk Turkanà kusini shule zote katika eneo hilo zimesalia kufungwa wiki chache tangu zifunguliwe.

Hofu inatokana na mwalimu wa kike wa shule ya Loyapata ambaye ni mjamzito kubakwa na wanaume wanne.

Sasa walimu wa shule hiyo wamehama kwa kuhofia usalama wao.

Hali hiyo ni sawa katika shule ya FILADEFIA ilioko kainuk ambapo darasa la wanafunzi 30 sasa lina wanafunzi watano pekee.

Mwalimu Peter Losike ambaye ndiye pekee alikuwa shuleni muda tukiwa pale amelalama akisema kwamba licha ya yeye kutoka katika maeneo ambayo yameathiriwa na usalama tena ameletwa katika hali hiyo.

Chifu Sara Lochodo ameiomba serikali kuongeza idadi ya walinda usalama kainuk maana wanawaangamiza watu barabarani na maafisa wa usalama  wako eneo hilo.  

Wakaazi wa kainuk wamekinzana na taarifa ya rais kuwa waziri wa usalama Kithure Kinduki amezuru maeneo hayo yaliyoathiriwa.

Hali eneo la kainuk ingali tete licha ya serikali kuongeza idadi ya maafisa.

Subscribe to eNewsletter