KAUNTI YA MARSABIT YALENGA KUHAKIKISHA SHERIA YA KUWALINDA WALEMAVU IMEBUNIWA KUFIKIA MWISHONI MWA MWAKA WA 2025.
December 3, 2024
Na Radio Jangwani
Maafisa wa polisi wanachunguza kisa cha wizi wa mifugo kilichotekelezwa jana eneo la Yamich lokesheni ya Shurr kaunti ya Marsabit.
Inadaiwa ngamia zaidi ya 350 walisafirishwa na wavamizi wasiojulikana ingawa hakuna majeruhi.
Mbunge wa North Horr Chachu Ganya amekashifu vikali tukio hilo na kutaka asasi za usalama kuharakisha uchunguzi wao kuhakikisha ngamia hao wanapatikana na kurejeshewa wenyewe ili kuzuia visa vya ulipishaji kisasi.
Kamishna wa kaunti ya Marsabit Paul Rotich anawataka wananchi kudumisha amani wakati polisi wakiendelea na operesheni ya kuwasaka na kuwakamata washukiwa wa visa vya uvamizi.