Local Bulletins

Utapiamlo waongezeka kwa asilimia 30 katika kaunti ya Marsabit makali ya kiangazi yakizidi kukaza

 

Na Silvio Nangori

Visa vya  utapiamlo miongoni mwa watoto katika kaunti ya Marsabit vinazidi kuongezeka Zaidi.

Kulingana na shirika la msalaba mwekundu ni kwamba hali hiyo ya utapiamlo imeongezeka kwa asilimia 30 watoto wakikosa kupata lishe bora.

Shirika hilo limesema kwamba hali ya sasa ipo mbaya zaidi na hivyo msaada wa dharura unahitajika ili kuwanasua wakaazi ambao wanazidi kuhangaishwa na makali ya kiangazi.

Mashirika tofauti yameanzisha miradi ya kuwanunua mifugo kutoka kwa wakaazi na kuwagawia wakaazi ili kupambana na kiangazi.

Hayo yanajiri huku Magavana wa kaunti za Kaskazini mwa Kenya wakitaka kiangazi katika maeneo hayo kutangazwa kuwa janga la kitaifa.

Magavana hao wakiongozwa na Ahmed Abdullahi wa Wajir, Mohamud Ali wa Marsabit, Nathif Jama  wa Garissa Mohamed Aden Khalif  wa Mandera maajuzi walitoa wito huo wakidai tangu ukame kutangazwa kuwa janga la kitaifa na rais mstaafu rais Uhuru Kenyatta mengi hayajafanyika.

Sasa wamemtaka Rais William Ruto kutangaza njaa katika eneo la kaskazini kuwa janga la kitaifa na kusaidia kuwanusuru wakaazi wa maeneo hayo.

Kaunti hizo hazijapokea mvua kwa misimu mitatu kufikia sasa.

Subscribe to eNewsletter