Local Bulletins

Waziri Sicily Kariuki asema madai ya njama ya kumuua naibu rais William Ruto yalikuwa ya uwongo

Waziri Sicily Kariuki, picha hisani.

Na Silvio Nangori

Waziri wa Maji, unyunyuziaji na usafi Sicily Kariuki amesema kwamba anawajibikia rais Uhuru Kenyataa Pekee ila si yeyote yule serikalini.

Kulingana na waziri huyo, ijapo ofisi yake yafaa kushirikiana kwa kiasi fulani na ile ya naibu wa rais basi maamuzi na maagizo yote yanatoka kwa rais mwenyewe.

Kariuki amemtaja Rais Uhuru Kenyatta kama mtu mkarimu na mwema kufanya kazi naye.

Hii ni baada ya kufanya kazi katika serikali ya Kenyatta katika wizara mbali mbali kama vile kwa wizara ya huduma kwa umma, vijana na maswala ya kijinsia, wizara ya afya na ile ya maji na sasa alipo.

Amekanusha madai kuhusika katika njama za kumuua naibu wa rais Willium Ruto mwaka wa 2019 kama inavyodaiwa na baadhi ya wafuasi wake. Amesema hizo zilikuwa habari za uwongo wa kupangwa.

Mwezi wa Juni mwaka wa 2019, Kariuki akiwemo na waziri wenzake kama vile John Mucheru wa mawasiliano na teknolojia na Peter Munya wa kilimo walishtumiwa kwa kupanga njama ya kumuua naibu wa rais William Ruto.

Comments are closed.

Subscribe to eNewsletter