Supkem Marsabit yaunga mkono wito wa kuwajibisha serikali ya Kenya Kwanza.
December 5, 2024
Na Emmanuel Amalo
Mwalimu mkuu wa chuo cha kati cha mafunzo ya ualimu Maria consolata katika jimbo Katoliki la isiolo Lmoti Emmanuel Ekisa amekamatwa kwa kukosa kulipia wanafunzi 30 usajili wa mitihani ya ECDE ambao ingeanza siku ya jumanne.
Inaaminika kuwa Mwalimu Mkuu huyo amepokea pesa shilingi 300,000 katika usajili wa wanafunzi kutoka mwezi wa Machi na Septemba hadi sasa pesa hizo hazijafika katika bodi ya mitihani (KNEC).
Mary Judy Ledeura ambaye ni mwanafunzi aliyeathirika amesema kuwa mwalimu mkuu huyo aliwaambiwa hawatafanya mtihani wao kwa sababu hakuweza kutuma pesa hizo kwa wakati.
Wanafunzi hao walishangazwa siku ya jumatatu baada ya kukosekana kwa wasimamizi wa mitihani kama ilivyokuwa matarajio yao.
Aidha waathiriwa pia wametoa hisia zao kusema muda wao umepotezwa huku wafanyakazi wa chuo hicho wakionekana kuacha shughuli yao kutokana na kutolipwa mishahara yao.
Taarifa ya polisi inasema kuwa Ekisa amekamatwa jana asubuhi na amepelekwa katika kituo cha polisi ya Isiolo kwa uchunguzi zaidi.