Wananchi Marsabit watakiwa kuchukua tahadhari wakati huu idara ya MET imetabiri mvua katika baadhi ya maeneo
Na Caroline Waforo
Wakaazi katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuchukua tahadhari wakati huu ambapo idara ya hali ya anga nchini MET imetabiri kuwa maeneo mengi jimboni yataendelea kupokea mvua.
Ni tahadhari ambayo imetolewa na kamanda wa polisi kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo ambaye pia amewataka wananchi kuepuka mikondo ya maji ili kuepuka hatari.
Vilevile madereva wametakiwa kuwa waangalifu barabarani kutokana na ukungu unaoshuhudiwa hasa nyakati za asubuhi huku Kamanda Kimaiyo akiwataka wananchi kuripoti visa vyovyote wakati huu wa mvua.
MET imetabiri kuwa baadhi ya maneo jimboni yatapokea mvua asubuhi, mchana na mvua inayoambatana na ngurumo nyakati za usiku.



Post Comment