Wamiliki na waendesha magari na Boda-boda mjini Marsabit kuanza kulipia ada ya maegesho hivi karibuni.
NA Samuel Kosgei
MANISPAA ya mji wa Marsabit inalenga kuanza kulipisha ada ya kuegesha magari mjini Marsabit katika kipindi cha mwezi mmoja ujao. Hayo ni kulingana na meneja wa manispaa ya Marsabit Boru Golicha.
Golicha akizungumza nasi baada ya mkutano wa pamoja uliowaleta pamoja wamiliki na wasimamizi wa magari ya usafiri, amesema kuwa hatua hiyo ni njia moja na kukusanya ushuru utaosaidia katika kukusanya pesa za maendeleo na pia kuleta nidhamu miongoni madereva wa magari.
Ameongeza kuwa sekta yao imepewa shabaha ya kukusanya shilingi milioni 20 katika mwaka mmoja wa kifedha.
Anasema pia wanalenga kufanya kikao na wamiliki na waendeshaji boda-boda na tuktuk ili kuwafahamisha sera zao mpya inayohusu kulipia pikipiki zao ada ya maegesho ambayo ni 200 kwa mwezi.
Msimamizi wa magari ya kampuni ya MEISO Shukri Huka amesema kuwa wao wamependekeza wasalie kwenye sehemu zao maegesho bila kuhamishwa. Pia wameomba ada ya magari ya yanayobeba abiria 10-14 ipunguzwe kutoka sh.2400 hadi sh.1500 kwa mwezi.
Aidha ameitaka manispaa ya Marsabit kuongeza vyumba vya choo katika steni mbali mbali ili kuepusha abiria wao kuhangaika.



Post Comment