Loading Now

Highlights

Wadau wa sekta ya haki Marsabit waanza kuchukua tahadhari dhidi ya ghasia kabla na baada ya uchaguzi wa 2027

Na Caroline Waforo

Wadau wa sekta ya haki katika kaunti ya Marsabit wameanza kuchukua hatua za tahadhari ili kuzuia ghasia zinazoweza kujitokeza kabla na baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Akizungumza baada ya mkutano wa watuamiaji wa mahakama yaani Court Users Committee uliofanyika mjini Marsabit hapo jana Alhmisi, Jaji wa mahakama kuu ya Marsabit Francis Rayola alisema kuwa wadau katika mfumo huo wa haki wanafuatilia kwa karibu matukio yanayoweza kuleta vurugu hasa kupitia matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

Jaji Rayola amesema kuwa idara mbalimbali zikiwemo mahakama, polisi na waendesha mashtaka zinaimarisha ushirikiano ili kukabiliana na vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha ghasia.

Na katika mkutano huo hofu ya matumizi ya dawa za kulevya kaunti ya Marsabit iliibuliwa huku sasa kamati hiyo ikipendekeza kuanzishwa kwa kituo cha kurekebisha tabia pamoja na kuanzishwa kwa wodi maalum ya huduma za afya ya akili katika Hospitali ya Rufaa na Mafunzo ya Marsabit ili kuwahudumia walio na magonjwa ya akili hasa kutokana na matumzi ya mihadarati na dawa za kulevya.

Kikao hicho huwaleta pamoja wadau mbalimbali wa sekta ya haki wakiwemo maafisa wa mahakama, polisi, ODPP, maafisa wa magereza, wanaharakati, viongozi wa kidini kati ya wadau wengine.

Post Comment