Highlights

Mwanaharakati Marsabit asema wanawake wanafaa kupata nafasi zaidi kwenye viti vya uongozi.

NA Nyabande Orwa

Huku kampeni za kuwania nafasi za kisiasa katika uchaguzi mkuu ujao zikianza kwa taratibu katika kaunti ya Marsabit, mwanaharakati wa kutetea uongozi bora na haki, Hassan Mohamed, amesema bado kuna changamoto kubwa katika kutoa nafasi za uongozi kwa kina mama.

Akizungumza na kituo hiki kwa njia ya simu, Hassan amesema jamii bado ina mtazamo kuwa mtoto wa kiume ndiye anayefaa kuongoza ikilinganishwa na mtoto wa kike. Aidha, anabainisha kuwa siasa za maelewano ni changamoto kubwa, kwani ni wanaume wanaoshirikishwa zaidi katika maamuzi makubwa ya jamii.

Hata hivyo, Hassan anasema bado kuna mwanga wa matumaini, kwa sababu katiba ya Kenya imetoa fursa kwa kina mama kushiriki katika uongozi kupitia viti vya wawakilishi wa wanawake. Mwanaharakati huyo ametoa wito kwa wanawake wengi kujitoa kwa wingi kuwania viti hivi, ili kupambana na dhana kwamba uongozi ni wa wanaume pekee.

Post Comment