Viongozi wapya wa muungano wa wafanyikazi wa umma Marsabit waahidi kutetea haki za wanachama
Na Nyabande Orwa
Viongozi wa Muungano wa wafanyikazi wa umma kaunti ya Marsabit wameahidi kulinda na kutetea maslahi ya wanachama wao kikamilifu.
Haya yamesemwa na Ali Kato aliyechaguliwa kuwa katibu mkuu wa tawi la muungano huo mjini Marsabit. Akizungumza na wanahabari siku moja baada ya uchaguzi huo, Kato ambaye alichaguliwa bila kupingwa, amesema kuwa uchaguzi ulikuwa wa amani huku wanachama wakijitokeza kwa wingi kuwachagua viongozi wao bila pingamizi.
Kato amesema viongozi wapya watahakikisha wanapigania mazingira bora ya kazi na kusawazishwa kwa mishahara ya wafanyikazi wa umma ili iwe sawa na wenzao katika serikali za kaunti.
Wakati huo huo, kiongozi wa kuwatetea kina mama katika muungano huo, Safia Katelo Doti, amesema yuko tayari kuhakikisha haki na nafasi za wanawake kazini zinalindwa na sauti zao zinasikika.



Post Comment