Uchaguzi wa 2027 utazingatia utendakazi wala si chama wala kabila,wasema vijana marsabit.
Na Nyabande Orwa
Vijana katika kaunti ya Marsabit wamesema katika uchaguzi mkuu wa 2027 watapiga kura kwa kuzingatia utendakazi wa viongozi, badala ya chama cha siasa au kabila.
Wakizungumza na kituo hiki mjini Marsabit, vijana hao pia wamelalamikia baadhi ya miradi inayotekelezwa na viongozi wa kaunti, wakisema haizingatii vipaumbele vya wananchi. Wametoa mfano wa ujenzi wa mabomba ya kupitisha maji taka katika maeneo ambayo hayana hata maji ya matumizi.
Aidha, vijana hao ambao wengi wao ni wahudumu wa bodaboda, wametoa wito kwa serikali ya kaunti kuwalipa wahudumu wa afya katika hospitali ya rufaa pamoja na wafanyakazi wasio wa kandarasi ya kudumu, wakisema hatua hiyo itaboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Wakati huo huo, mwakilishi wa wadi ya Karare, Joseph Leruk, amewahimiza wananchi kuwachagua viongozi katika uchaguzi wa 2027 kwa kuzingatia utendakazi wa kila mmoja, badala ya kuwahukumu viongozi wote kwa pamoja.



Post Comment