Mwanamume afungwa miaka 10 Jela kwa Kumtishia babake kwa kisu Marsabit
Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 27 amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela kwa kosa la kumtishia kumuua babake katika kijiji cha Majengo, Marsabit ya Kati.
Mahakama imelezwa kuwa mshukiwa, Hassan Molu Kuno, alimtishia babake, Molu Kuno Sora, kwa kutumia kisu na rungu baada ya kutokea mzozo kuhusu suala la kuchuna miraa shambani.
Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Marsabit, Christine Wekesa. Tukio hilo lilitokea tarehe 3 Januari mwaka huu.
Mahakama pia ilibaini kuwa hii si mara ya kwanza kwa kuno kutuhumiwa kwa kosa kama hilo. Molu ana siku kumi na nne kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.



Post Comment