Highlights

Mwanamume afungwa miaka 10 Jela kwa Kumtishia babake kwa kisu Marsabit

Mwanamume mmoja mwenye umri wa miaka 27 amehukumiwa kifungo cha miaka kumi jela kwa kosa la kumtishia kumuua babake katika kijiji cha Majengo, Marsabit ya Kati.

Mahakama imelezwa kuwa mshukiwa, Hassan Molu Kuno, alimtishia babake, Molu Kuno Sora, kwa kutumia kisu na rungu baada ya kutokea mzozo kuhusu suala la kuchuna miraa shambani.

Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Marsabit, Christine Wekesa. Tukio hilo lilitokea tarehe 3 Januari mwaka huu.

Mahakama pia ilibaini kuwa hii si mara ya kwanza kwa kuno  kutuhumiwa kwa kosa kama hilo. Molu ana siku kumi na nne kukata rufaa kupinga hukumu hiyo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment