Loading Now

Highlights

Maafisa wa gereza la Marsabit watibua jaribio la mshukiwa mmoja kutoroka

Na Caroline Waforo

Maafisa wa gereza la Marsabit wametibua jaribio la mshukiwa mmoja kutoroka, katika kisa cha leo Jumatatu.

Akizungumza na Shajara Afisa Msimamizi wa gereza la Marsabit Hussein Guyo, amesema kuwa mshukiwa huyo wa karibia miaka 30 alijaribu kutoroka alipokuwa katika mazingira ya Mahakama ya Marsabit ambapo anakabiliwa na kesi ya kutishia kuua.

Wakati wa jaribio hilo, maafisa wa magereza walikabiliana na mshukiwa huyo na kumzuia kutoroka.

Mshukiwa huyo alinaswa na yuko katika gereza hilo la Marsabit huku Guyo akisema kuwa uchunguzi umeanzishwa ili kubaini sababu zilizochochea mwanaume huyo kujaribu kutoroka.

Kutokana na jaribio hilo mshukiwa anakodolea macho shtaka jingine la kujaribu kutoroka.

Post Comment