Loading Now

Highlights

Kamishna wa Marsabit James Kamau atoa onyo kali kwa wezi wa mifugo 

Na Carolina Waforo

Kamishna wa kaunti ya Marsabit James Kamau ametoa onyo kali kwa wafugaji dhidi ya kujihusisha katika visa vya wizi wa mifugo.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake Kamishna Kamau amedokeza kuwa pameibuka visa na ambao wafugaji waliohamia maeneo mengine kwa ajili ya kusaka malisho msimu wa kiangazi sasa wanarejea makwao msimu huu wa mvua ambapo baadhi yao wameripotiwa kuhusika katika visa vya wizi wa mifugo.

Ameonya kuwa kamati za malisho zitalazimika kuwanyima wanaotekeleza visa hivyo nafasi za kulisha katika maeneo husika.

Na huku mvua ikiendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali jimboni Marsabit, Kamishana Kamau amewahimiza wananchi kupanda miche.

Vile amewasishi wafugaji kujihusisha katika njia mbadala za mapato huku akiwahimiza wakulima kutumia kipindi hichi cha mvua kwa upanzi wa mazao yao.

Post Comment