Highlights

Idara ya kilimo Marsabit yahimiza wakulima kuchangamkia mvua za mapema.

Na Samuel Kosgei

Wakulima katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuchangamkia msimu wa mvua unaoonekana kuanza mapema kwa kuanza kupanda mazao mashambani.

Akizungumza na kituo hiki, Afisa wa Kilimo katika kaunti ndogo ya Marsabit Central, Duba Nura, amesema huu ni wakati mwafaka kwa wakulima kupanda mazao hasa yale yanayokomaa kwa muda mfupi.

Amewahimiza pia kutumia mbegu bora zinazoendana na hali ya hewa ya eneo hilo ili kuongeza uzalishaji.

Wakati huo huo, Nura amewataka wakazi wanaopokea mvua kwa sasa kuvuna na kuhifadhi maji ya kutosha ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji wakati wa kiangazi.

Aidha, amewahimiza wafugaji kuwapa mifugo yao chanjo na dawa za kuzuia magonjwa yanayoweza kuibuka msimu huu wa mvua na baridi, akibainisha kuwa mifugo mingi bado inadhoofika kutokana na athari za kiangazi kilichopita.

Amewashauri wafugaji kutafuta ushauri zaidi kutoka kwa maafisa wa idara ya mifugo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment