Familia zaidi ya 100 katika eneo la Saku wafaidika na chakula cha msaada kutoka kwa kanisa la AIC Marsabit
Na JB Nateleng
Angalau familia zaidi ya 100 katika eneo la Saku wameweza kufaidika na chakula cha msaada kutoka kwa kanisa la AIC Marsabit.
Akizungumza na idhaa hii mchungaji wa kanisa hilo Reverend William Godana amesema kwamba chakula hichi kitawasaidia wakazi hawa katika kupambana na makali ya kiangazi ambayo yanaendelea kushuhudiwa katika kaunti nzima ya Marsabit.
Amesema kwamba wamekuwa wakilenga familia zisizojiweza kimapato pamoja na wale wakongwe katika jamii ili kuwapa chakula cha kuwasitiri wakati huu wa kiangazi huku akitoa wito kwa serekali pamoja na mashirika yasiyo ya kiserekali kuweza kutuma msaada zaidi.



Post Comment