Baadhi ya maeneo kaunti ya Marsabit kuendelea kupokea mvua katika kipindi cha siku saba zijazo
Na Caroline Waforo
Utabiri wa hali ya hewa katika kipindi cha siku saba zijazo kuanzia leo tarehe 3 mwezi Machi hadi 9 Machi 2026 unaonyesha kuwa baadhi ya maeneo katika Kaunti ya Marsabit yatapokea mvua nyakati za asubuhi, mchana na mvua itakayoambatana na ngurumo nyakati za usiku.
Kulingana na ripoti hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa idara ya hali ya hewa MET, kaunti ya Marsabit John Nguyo, kijibaridi cha asubuhi kinatarajiwa katika maeneo ya Saku, Ngurunit na Mt Kulal.
Aidha, baadhi ya maeneo jimboni yanatarajiwa kupokea upepo wastani hadi mkali kutoka kusini hadi kusini-mashariki.
Hata hivyo, maeneo mengi ya Loyangalani yanatarajiwa kukumbwa na upepo mkali sana.
Na kufuatia mvua inayonyesha kwa sasa wakulima wamehimizwa kutumia kipindi hiki kupanda mimea yao.



Post Comment