Highlights

Akina mama Marsabit wahimizwa kuwa mabalozi wa amani

Na JB Nateleng

Akina mama katika kaunti ya Marsabit wametakiwa kuwa mabalozi wa amani ili kuimarisha utulivu na mshikamano miongoni mwa jamii zinazoishi jimboni.

Wito huo umetolewa na Chifu Joy Lenawalbene kutoka Kaunti ya Samburu, ambaye amesema kuwa wanawake wana ushawishi mkubwa katika jamii na wana nafasi muhimu ya kuwahamasisha vijana pamoja na wazee kuhusu umuhimu wa kudumisha amani.

Akizungumza siku ya hapo jana Jumapili wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika katika eneo la Gadamoji katika eneo bunge la Saku, Chifu Lenawalbene amewahimiza wanawake kuhubiri amani hasa katika kipindi hiki ambapo joto la kisiasa linendelea kushuhudiwa nchini.

Aidha, Chifu Lenawalbene amewataka akina mama kupigania haki ya ardhi yao kusajiliwa kama ardhi ya jamii ili, waweze kunufaika na miradi ya maendeleo itakayowekezwa katika maeneo yao.

Wakati huo huo, Kamishna Msaidizi wa lokesheni ya Diri, Martin Buluma, amesema serikali inaendelea kuweka juhudi kuhakikisha haki za wanawake zinalindwa kote nchini.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment