Wazee waliokamatwa Marsabit kuzuiliwa kwa siku 10, wadaiwa kushirikiana na Oromo Liberation Army
Na Mwandishi Wetu
Wazee wawili waliokamatwa siku ya Jumamosi katika kaunti ya Marsabit watazuiliwa kwa siku 10, hii ni baada ya kufikishwa katika mahakama ya Kahawa hapo jana Jumatatu.
Aliyekuwa chifu wa Golole, Dabassa Dambi, alikamatwa kutoka nyumbani kwake mjini Sololo huku Mzee Guracha Dambala akikamatwa katika eneo la Archers Post alipokuwa akisafiri kuelekea Nairobi.
Kumatawa kwao kulizua madai ya utekaji nyara na kupelekea wakaazi wa Sololo kuandamana na kufunga barabara kuu ya Marsabit-Moyale siku ya Jumapili.
Upande wa mashtaka ulieleza Mahakama kuwa wawili hao walikamatwa kufuatia operesheni ya kiusalama na kutupilia mbali madai ya utekaji nyara.
Mwendesha Mashtaka Harrison Kiarie, aliambia mahakama kuwa wawili hao wanahusishwa na kundi la Oromo Liberation Army kutoka nchini Ethiopia, wakidaiwa kushirikiana na kundi hilo katika kupanga njama ya uvamizi katika eneo la Basir na Sololo.
CUE IN…PRESECUTOR ON ARMY
Upande wa mshtaka uliomba siku 30 kukamilisha uchunguzi, ila mahakama ikatoa siku 10 pekee.
Mahakama pia iliamuru wawili hao kuzuiliwa katika kituo chenye uwezo wa kutoa huduma za matibabu.
Kesi hiyo itatajwa tarehe 22 mwezi huu wa Mei



Post Comment