Highlights

Wakazi Marsabit wahimizwa kupinga dhulma dhidi ya wanawake

Na Joy Akinyi & JB Nateleng

Wakazi wa kaunti ya Marsabit wametakiwa kuachana na vitendo vya dhulma dhidi ya wanawake katika jamii.

Wito huo umetolewa na Sheikh wa Msikiti wa Jamia Marsabit, Sheikh Mohamed Noor, ambaye amesema baadhi ya jamii za wafugaji bado zinaendeleza mila na desturi zinazowanyima wanawake haki zao.

Sheikh Noor amesema vitendo vya dhulma dhidi ya wanawake vinadhoofisha maendeleo ya jamii na kuathiri ustawi wa familia.

Amehimiza viongozi mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na viongozi wa dini kushirikiana katika kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kulinda haki za wanawake.

Aidha, Sheikh Noor ametaja ukeketaji wa watoto wa kike kuwa moja ya vitendo vya ukatili vinavyopaswa kukomeshwa mara moja akisema kuwa ukeketaji haukubaliki kidini wala kisheria huku akiwataka wanaoendeleza mila hiyo kuachana nayo na badala yake kulinda afya na maisha ya watoto wa kike.

Kauli yake inajiri siku moja baada ya ulimwengu kuadhimisha Siku ya Akina Mama Duniani ambayo uadhimishwa jumapili ya pili ya mwezi wa tano kila mwaka kwa lengo la kuwaenzi kina mama kwa zawadi, na mikusanyiko ya familia.

Post Comment