Highlights

Wazee wa jamii ya Borana, Moyale wataka kuachiliwa kwa wazee wawili wanaozuiliwa

Na Mwandishi wetu

Wazee wa jamii ya Borana kutoka eneo-bunge la Moyale kaunti ya Marsabit wameitaka serikali kuingilia kati na kuamuru kuachiliwa mara moja kwa wazee wawili waliokamatwa siku ya Jumamosi kwa madai ya kushirikiana na kundi la Oromo Liberation Army, katika njama ya kupanga uvamizi katika eneo la Basir linalozozaniwa.

Katika taarifa ya pamoja leo Jumatano ambayo imesomwa na Mzee Hajji Hussein Kadida, wazee hao wamekashifu idara ya usalama kwa kile wanadai ni kukamatwa na kuzuiwa kwa wazee wasiokuwa na hatia.

Aidha wameomba mkao na Rais William Ruto ili waweze kuwasilisha lalalama zao

Wakati uo huo, wazee hao ameitaka serikali kusuluhisha kwa haraka mzozo wa umiliki wa ardhi inayozozaniwa ya Basir mpakani mwa Marsabit na Wajir.

Itakumbukwa kuwa aliyekuwa chifu wa Golole, Dabassa Dambi, alikamatwa kutoka nyumbani kwake mjini Sololo huku Mzee Guracha Dambala akikamatwa katika eneo la Archers Post alipokuwa akisafiri kuelekea Nairobi ambapo walifikishwa katika mahakama ya Kahawa siku ya Jumatatu.

Mahakama iliamuru wawili hao kuzuiliwa kwa siku 10 ili kutoa nafasi ya uchunguzi.

Kesi hiyo itatajwa tarehe 22 mwezi huu wa Mei

Post Comment