Wakazi wa Marsabit walalamikia kutotekelezwa kwa miradi wanayopendekeza katika mikutano ya kutoa maoni kuhusu bajeti.
Na Samuel Kosgei
Wakazi wa kaunti ya Marsabit leo Alhamisi waliwasilisha mapendekezo yao ya miradi ya maendeleo ya maeneo bunge kwa mwaka wa kifedha wa 2026/2027.
Kikao hicho kiliwakutanisha wawakilishi kutoka maeneo bunge ya Saku, Laisamis, Moyale na North Horr.
Zoëzi hilo linaongozwa na Kamati ya Bunge la Kitaifa kuhusu Bajeti na Matumizi ya Fedha ikiongozwa na mbunge wa Samburu West Naisula Lesuuda kwa ushirikiano na Joseph Lekuton pamoja na Mathias Robi.
Akizungumza katika kikao hicho kilichoandaliwa mjini Marsabit, mbunge wa Laisamis Joseph Lekuton aliwahakikishia wananchi kuwa miradi muhimu itakayopendekezwa itazingatiwa na kutekelezwa.
CUE IN… LEKUTON ON BUDGET
Hata hivyo, baadhi ya wazungumzaji wakiongozwa na Abdikadir, mfanyabiashara kutoka Saku, walidai kuwa licha ya wananchi kuendelea kupendekeza miradi mbalimbali, mingi bado haijatekelezwa. Walitaka kamati hiyo kuhakikisha ahadi za awali zinatimizwa kabla ya kuanzishwa kwa miradi mipya.
CUE IN… ABDIKADIR
Kwa mujibu wa kamati hiyo, kila eneo bunge katika kaunti ya Marsabit limetengewa shilingi milioni mia moja, huku wananchi wakitakiwa kutaja miradi wanayotaka kupewa kipaumbele.



Post Comment