Highlights

Wakazi Marsabit watoa hisia mseto kuhusu mswada wa Ajira

Na Abdiaziz Yusuf

Siku chache baada ya seneta wa kaunti ya marsabit Mohamed Chute kuwasilisha mswada ya kuanzishwa kwa bodi maaluma ya kutoa ajira kwa wakenya.

Wakaazi wa kaunti ya Marsabit wamepongeza mswada huo wakidai kuwa ni hatua itakayosaidia kupunguza ukabila na ufisadi

Wakizungumza na shajara wakazi hao wamesema ni mchakato wa ajira utawasidia jamii ya wafugaji ambayo kwa muda mrefu wamekumbwa na changamoto ya ukabila.

Hata hivyo, baadhi yao wameeleza wasiwasi wao wakihofia kuwa huenda wabunge wasipitishe mswada huo, wakidai kuwa unaweza kupunguza ushawishi wao katika masuala ya ajira, hususan kuwapa nafasi watu wanaotoka maeneo yao.

Post Comment