Highlights

Utafiti waonyesha kwamba asilimia kubwa ya Wakenya wanaimani na utendaji wa wanahabari.

Na JB Nateleng

Utafiti uliofanyika umebaini kuwa asilimia 79 ya Wakenya wana imani na utendaji wa wanahabari nchini.

Haya yamejiri katika kongamano lililoandaliwa na Baraza la Vyombo vya Habari Kenya (MCK) leo, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani.

Katika kongamano hilo, MCK imeeleza kuwa wanahabari wana jukumu muhimu la kuelimisha wananchi kuhusu haki zao na pia kuwasukuma viongozi kutekeleza majukumu yao kwa uwazi na ufanisi.

Kauli hiyo imeungwa mkono na Mratibu wa MCK eneo la Kati na Mashariki, Jackson Karanja, ambaye amesema wanahabari wanapaswa kupewa uhuru wa kutosha ili waweze kutekeleza kazi zao kwa weledi na uadilifu.

Karanja pia amesema kumekuwepo na visa vya baadhi ya taasisi za serikali kuwanyima wanahabari taarifa, hatua ambayo amesema inazuia haki ya upatikanaji wa habari.

Aidha, amewataka wanasiasa na wananchi kutumia njia sahihi za kisheria kuwasilisha malalamishi dhidi ya wanahabari badala ya kuchukua sheria mikononi mwao, akisisitiza kuwa hilo halikubaliki kisheria.

Pia amewataka wanahabari kuwa waangalifu wanapotekeleza majukumu yao, hasa katika kipindi hiki ambacho nchi inaelekea katika uchaguzi mkuu.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment