Highlights

Wakaazi mjini Marsabit waunga mkono pendekezo la muungano wa KUCO la kuhamishwa kwa huduma za afya hadi serikali kuu

Na Sabalua Moses

Baadhi ya wakaazi mjini Marsabit wameunga mkono pendekezo la muungano wa maafisa wa kliniki KUCO la kuhamishwa kwa huduma za afya kutoka serikali za kaunti hadi serikali kuu.

Wakizungumza na Shajara wakaazi hao wamesema kuwa hatua hiyo itapunguza migomo ya mara kwa mara katika kaunti mbalimbali na hivyo kuboresha utoaji wa huduma za afya.

Wamesema kuwa hatua hiyo inaweza kuhakikisha malipo ya wakati na mazingira bora ya kazi kwa maafisa wa kliniki.

Aidha baadhi ya wakaazi wamepinga pendekezo hilo na kuzitaka serikali za kaunti kuwajibika katika majukumu yao na kuboresha huduma za afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora.

Viongozi wa muungano wa KUCO walitoa wito huo hapo jana Jumatano baada ya kutia saini rasmi makubaliano ya kurejea kazini kwa maafisa wa kliniki Marsabit na serikali ya kaunti, hatua iliyokomesha mgomo uliodumu kwa siku 217.

Post Comment