Wakaazi Marsabit waendelea kuonywa dhidi ya dhulma za kijinsia
Na Caroline Waforo
Siku moja baada ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wakaazi katika kaunti ya Marsabit wameendelea kuonywa dhidi ya dhulma za kijinsia.
Akizungumza na Shajara Kamanda wa polisi katika kaunti ya Marsabit Leonard Kimaiyo amesema kuwa dhulma hizi zinazojumuisha ukeketaji pamoja na ndoa za mapema bado zinashuhudiwa miongoni mwa jamii hasa baada ya kisa na ambapo mwanafunzi wa miaka 14 alipachikwa mimba na sasa ni mzazi wa mtoto wa miezi sita katika lokesheni ya Nairibi eneobunge la Laisamis.
Kamanda Kimaiyo amesema kuwa msichana huyo wa gredi ya 8 kutoka shule ya msingi Nairibi aligundulika baada yake kukosa kuripoti shuleni kwa ajili ya gredi ya 9 jambo lililopelekea walimu kutaka kujua sababu yake ya kutoripoti shuleni.
Kamanda Kimaiyo amesema kuwa mshukiwa aliyemtunga mimba mwanafunzi huyo bado anaendelea kusakwa na maafisa wa usalama.
Vilevile amewataka wananchi kuhakikisha kuwa wanaheshimu haki za kila mmoja katika jamii.



Post Comment