Viongozi wa marsabit watakiwa kuzungumzia mijadala ya kitaifa badala ya kukimya huku wakaazi wakiathirika.
Na Samuel Kosgei
Viongozi wa Marsabit wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuzungumzia masuala ya kitaifa badala ya kukaa kimya huku wakaazi wakiumizwa na sera za serikali ya kitaifa.
Akizungumza na kituo hiki wakili kutoka mjini Marsabit John Behailu ambaye pia ni mwaniaji wa kiti cha ubunge Saku mwaka ujao amesema wabunge wa Marsabit wanapaswa kutoa sauti zao akibainisha kuwa Marsabit ni mojawapo ya kaunti zilizoathirika zaidi kutokana na umbali wake hali inayochangia kupanda kwa gharama ya mafuta. Behailu amewataka viongozi hao kushiriki kikamilifu katika mijadala ya kitaifa na kutafuta suluhu bungeni, akisisitiza kuwa ni wajibu wao kuhakikisha kilio na matatizo ya wakazi wa Marsabit yanasikika na kushughulikiwa.



Post Comment