Highlights

Mtoto wa siku moja aliyetupwa aokotwa viungani mwa mji wa Marsabit.

Na Abdilaziz Yusuf

Mtoto mchanga wa siku moja amepatikana aliyetupwa na mamake ameokolewa katika eneo la Bank Quarter mjini Marsabit.

Mtoto huyo wa kiume alipatikana mapema Jumatatu asubuhi majira ya saa tisa na Yusuf Woche aliyekuwa akitoka kazini katika eneo hilo.

Akithibitisha kisa hicho, OCPD wa Marsabit Central Beethoven Gachago amesema polisi wameanzisha uchunguzi ili kubaini aliyemtupa mtoto huyo.

Aidha ametoa wito kwa wananchi wenye taarifa zozote zinazoweza kusaidia kubaini mamake mtoto huyo kujitokeza na kushirikiana na idara ya polisi ili wamsaidie mtoto huyo.

Hata hivyo amesema kwa sasa polisi wanashirikiana na makao ya kuwahudumia watoto, Children Rescue Home, kuhakikisha mtoto huyo anapata huduma na uangalizi unaohitajika huku uchunguzi ukiendelea.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment