Usalama waimarishwa Marsabit kuelekea sikukuu ya Eid-Al-Adha
Idara ya usalama katika kaunti ya Marsabit imewahakikishia wakaazi usalama wa kutosha wakati wa sherehe za sikukuu ya Eid-Al-Adha hapo kesho Jumatano.
Akizungumza na Shajara Kamanda wa polisi Marsabit Leonard Kimaiyo, amesema kuwa maafisa wa polisi wameimarisha doria kote jimboni ili kuhakikisha kuwa waumini wa dini ya Kiislamu wanasherehekea kwa amani na utulivu.
Aidha amewahimiza wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa mapema kuhusu mienendo yoyote ya kutiliwa shaka ili kuzuia visa vya uhalifu.
Hapo jana Jumatatu Serikali ilitangaza kesho Mei 27, kuwa siku kuu ya Eid al-Adha, hivyo basi kuwa siku ya mapumziko.
Siku kuu hiyo huadhimishwa na Waislamu kuashiria kukamilika kwa safari ya Hajj mjini Mecca.
Eid- Al- Adha ni sherehe ya kumbukumbu ya kafara ya mtoto aliyotoa Mtume Abraham, kwa Mungu kuashiria heshima yake.
Siku hii husherekewa na Waislamu kwa kuchinja mifugo na kugawana nyama na wasiojimudu katika jamii.
Üsküdar Su Kaçağı Tespiti Yapan Firmalar
Ok!



1 comment