Highlights

Papa Leo XIV amteua Padri John Mbua Mwandi kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kitui

Waamini wa Kanisa Katoliki nchini Kenya wamepokea kwa furaha uteuzi wa Padri John Mbua Mwandi kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo Katoliki la Kitui, baada ya tangazo rasmi kutoka Vatican kupitia Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Holy See.

Hadi uteuzi wake Padri John Mbua alikuwa Padri mkuu wa Parokia ya Mulutu.

Askofu Mteule John Mbua Mwandi alizaliwa tarehe 24 Septemba 1970. Alisoma falsafa katika Seminari Kuu ya Saint Augustine iliyoko Jimbo katoliki la Bungoma, na baadaye akasomea theolojia katika Seminari Kuu ya Saint Matthias Mulumba iliyoko Kapsabet.

Alipadrishwa tarehe 8 Desemba 2001.

Baada ya kupadrishwa, Askofu Mteule Mwandi alihudumu katika nyadhifa mbalimbali ndani ya Kanisa. Alianza kama Paroko Msaidizi wa Ikutha mwaka 2002, kisha akawa Paroko wa Miambani, Ikanga, na baadaye Kanisa Kuu (Cathedral) ya Kitui.

Katika huduma yake ya kichungaji, alihitimu stashahada ya Usimamizi wa Miradi kutoka Kenya Institute of Management, Nairobi, mwaka 2008. Kuanzia mwaka 2011 hadi 2020, alihudumu kama Mhasibu wa Jimbo kisha akaendelea kuwa vika jenerali wa Jimbo Katoliki la Kitui. 

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

5 comments

comments user
Üsküdar Mutfak Su Kaçağı Tespiti

Üsküdar Mutfak Su Kaçağı Tespiti Kaçak tespit raporu mahkeme dosyası için geçerli oldu.

comments user
Üsküdar Pis Su Kaçağı Tespiti

Üsküdar Pis Su Kaçağı Tespiti Üsküdar su kaçağı tespiti hizmeti güven verdi

comments user
Üsküdar Zemin Altı Su Kaçağı Tespiti

Üsküdar Zemin Altı Su Kaçağı Tespiti Duvar içindeki kaçak noktasal olarak bulundu.

comments user
Üsküdar Garantili Su Kaçağı Tespiti

Üsküdar Garantili Su Kaçağı Tespiti Nokta atışı tespit sayesinde gereksiz masraf olmadı.

comments user
Üsküdar Su Kaçağı Bulma

Üsküdar Su Kaçağı Bulma Nişantaşı sınırındaki evime gelmeleri sadece 45 dakika sürdü.

Post Comment