Loading Now

Highlights

Shirikisho la Soka (FKF) tawi la Marsabit latangaza rasmi kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho kwa wachezaji.

Na JB Nateleng

Shirikisho la Soka (FKF) tawi la Marsabit limetangaza rasmi kufunguliwa kwa dirisha la uhamisho kwa wachezaji katikati ya msimu ambao umeanza rasmi leo Jumatatu hadi tarehe 20 mwezi huu wa Machi 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na FKF tawi la Marsabit dirisha hilo la uhamisho litadumu kwa siku 19 likitarajiwa kusaidia vilabu katika kujiandaa ipasavyo kwa kusajili wachezaji wenye tajriba ambao watawasaidia katika kujiandaa kwa msimu utakaorejelewa tarehe 28 Machi 2026.

Hata hivyo kwenye dirisha hili kila klabu itaruhusiwa kuachilia na kusajili wachezaji wasiozidi watatu na kila klabu inaweza kusajili hadi wachezaji wanne huru (free agents).

Aidha shirikisho hili limehimiza kuwa lazima uhamisho ufuate utaratibu rasmi wa mtandaoni na ushirikishe klabu huku ikisisitiza kwamba hakuna mchezaji atakayeruhusiwa kuondoka bila idhini ya klabu chake, kwa kuwa wachezaji wote waliosajiliwa wamefungwa na vilabu vyao hadi Juni 2026.

Itakumbukwa kwamba shirikisho la soka tawi la Marsabit liliahirisha michezo zote kwa sababu ya mfungo wa Ramadhani hadi tarehe 28 Machi 2026.

Post Comment