Highlights

RUSA yakashifu wizi wa mifugo Kambinye

Na Sabalua Moses

Muungano wa wanafunzi wa vyuo vikuu kutoka jamii ya Rendille chini ya chama cha (RUSA) umekashifu vikali tukio la wizi wa mifugo lililotokea wiki iliyopita katika eneo la Kambinye, wadi ya Kargi.

Wakizungumza na wanahabari, naibu mwenyekiti wa chama hicho Jordan Sahado amesema kuwa wizi wa mifugo ni uhalifu usio na kabila, akisisitiza kuwa hakuna mila yoyote inayounga mkono vitendo vya wizi wa mifugo.

Sahado pia amelaani uharibifu wa mali na mifugo uliosababishwa na tukio hilo, akieleza kuwa uhalifu huo umeathiri pakubwa maisha ya wafugaji wanaotegemea mifugo kama njia kuu ya kujikimu katika eneo hilo.

Radio Jangwani 106.3FM is a community radio station situated in Marsabit County broadcasting from Marsabit town. It is the brain child of the bishop of catholic diocese of Marsabit, Rt. Rev. Peter Kihara. It is established with the objective of reaching the people Marsabit diocese and Marsabit County for evangelization, Education, entertaining and disseminating information to the masses.

Post Comment